DC mzava akabidhi mwenge wa uhuru 2026 mwanga
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Same Godfrey Mzava leo Juni 29, 2026 amemkabidhi Mwenge wa Uhuru 2026 Kwa kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Hassan Bomboko katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye Uwanja wa mgagao
Makabidhiano hayo yanaashiria kukamilika kwa mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Same na kuanza rasmi kwa mbio hizo katika Wilaya ya Mwanga, ambapo mwenge utatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mzava amesema Mwenge wa Uhuru unaendelea kuwa chombo muhimu cha kuhimiza uwajibikaji, uzalendo na usimamizi wa miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi.
Kwa upande wake, bomboko ameahidi kuendeleza mbio za Mwenge wa Uhuru kwa kuzingatia ratiba iliyopangwa, huku akiwataka wananchi wa Mwanga kujitokeza kushiriki katika shughuli mbalimbali zitakazoambatana na mbio hizo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa Serikali, watumishi wa umma, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi, waliojitokeza kushuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika kwa utaratibu na heshima.

No comments