Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

ad728

TANESCO KIGAMBONI YASONGEZA HUDUMA KARIBU KWA WATEJA

Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kigamboni, Bi. Tumaini  Mahwaya akizungumza na Wafanyakazi wa Hoteli ya Aya Sophia, Kigamboni wakati akitoa elimu ya hudumba  mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo leo Julai 28, 2026, Dar es Salaam

Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Wilaya ya Mikwambe, Godwin Marandu akitoa elimu kwa Wafanyakazi wa Hoteli ya Aya Sophia iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam

Afisa Uhusiano wa Huduma kwa Wateja TANESCO Wilaya ya Kimbiji, Henry Martin akitoa elimu kwa Wafanyakazi wa Hoteli ya Aya Sophia iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam

Wafanyakazi wa Hoteli ya Aya Sophia wakipewa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia

Wafanyakazi wa Hoteli ya Aya Sophia wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Kigamboni

.........

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kigamboni limeendelea kusogeza huduma karibu na wateja kwa kutoa elimu kwa wafanyakazi wa Hoteli ya Aya Sophia, iliyopo Kata ya Somangila, kuhusu huduma mbalimbali za shirika pamoja na matumizi salama ya umeme.

Katika elimu hiyo iliyotolewa leo, Julai 28, 2026, wafanyakazi walipatiwa ufafanuzi kuhusu huduma za kidijitali za TANESCO ikiwemo LUKU Kijanja, MCHONGO 180 na NIKONEKT JISOTI, sambamba na kuhamasishwa kutumia nishati safi ya kupikia na kushiriki katika ulinzi wa miundombinu ya umeme.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Kigamboni, Bi. Tumaini Mahwaya, amesema shirika linaendelea kuboresha huduma zake ili kuhakikisha wateja wanapata umeme wa uhakika na huduma kwa urahisi.

Amesema pamoja na maboresho ya huduma, TANESCO inaendelea kutekeleza mpango wa kuongeza transfoma katika Mkoa wa Kigamboni kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa umeme na kukidhi ongezeko la mahitaji ya wananchi.

Mahwaya amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda miundombinu ya umeme kwa kutoa taarifa wanapobaini vitendo vya wizi au uharibifu, akibainisha kuwa miundombinu hiyo ni mali ya taifa yenye gharama kubwa za ujenzi na matengenezo.

Aidha, amesisitiza matumizi ya njia rasmi za mawasiliano na TANESCO, ikiwemo huduma ya MCHONGO 180, ili kurahisisha utoaji wa taarifa za hitilafu, maombi ya huduma na dharura.

Kwa upande wake, Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Wilaya ya Mikwambe, Godwin Marandu, ameeleza faida za huduma za kidijitali za TANESCO, akiwahamasisha wateja kutumia LUKU Kijanja na NIKONEKT JISOTI ili kupata huduma kwa haraka na kwa ufanisi.

Naye Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Wilaya ya Kimbiji, Henry Martin, amesisitiza umuhimu wa kuzingatia kanuni za usalama katika matumizi ya umeme majumbani na maeneo ya kazi ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.

Wakizungumza baada ya kupokea elimu hiyo, wafanyakazi wa Hoteli ya Aya Sophia wamepongeza TANESCO kwa kuwafikia na kuwapatia uelewa kuhusu huduma zake, wakisema elimu hiyo itawasaidia kutumia umeme kwa usalama na kufahamu njia sahihi za kupata huduma na kutoa taarifa wanapokumbana na changamoto..

Post a Comment

0 Comments