
Mkurugenzi wa Kitengo cha Nishati Safi ya Kupikia kutoka Wizara ya Nishati, Nolasco Mlay akizungumza katika hafla ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambuliwa kama Kinara wa Nishati Safi Afrika iliyofanyika leo Agosti 7, 2026, jijini Dar es Salaam.

Mhandisi wa Miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Raya Majallah, akizungumza katika hafla ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambuliwa kama Kinara wa Nishati Safi Afrika iliyofanyika leo Agosti 7, 2026, jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Subira Mgalu, akizungumza katika hafla ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambuliwa kama Kinara wa Nishati Safi Afrika iliyofanyika leo Agosti 7, 2026, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa WYFI na Mbunge Viti Maalum ( CCM), Mhe. Asha Baraka, akizungumza katika hafla ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambuliwa kama Kinara wa Nishati Safi Afrika iliyofanyika leo Agosti 7, 2026, jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Elimu kwa Walipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), CPA Paul Walalaze, akizungumza katika hafla ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambuliwa kama Kinara wa Nishati Safi Afrika iliyofanyika leo Agosti 7, 2026, jijini Dar es Salaam.


........
Serikali imeitaka jamii kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati safi ya kupikia, ikiwemo uzalishaji, usambazaji na matumizi ya teknolojia za kupikia kwa kutumia umeme, gesi, bayogesi na majiko banifu, hatua itakayosaidia kuongeza kipato cha wananchi na kuchochea maendeleo ya taifa.
Akizungumza leo, Agosti 7, 2026, jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, katika hafla ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutambuliwa kama Kinara wa Nishati Safi Afrika, Mkurugenzi wa Idara ya Nishati Safi ya Kupikia kutoka Wizara ya Nishati, Nolasco Mlay, amewahimiza wanawake na vijana kutumia fursa zilizopo katika sekta ya nishati safi ya kupikia ili kuinua uchumi wao.
Mlay amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameifanya ajenda ya nishati safi ya kupikia kuwa ajenda ya kitaifa, kikanda na kimataifa kupitia uongozi wake unaohamasisha matumizi ya nishati safi kwa maendeleo endelevu.
"Chini ya uongozi wa Rais Samia, matumizi ya nishati safi ya kupikia hayatazamwi tena kama suala la jikoni pekee, bali ni ajenda inayogusa afya ya jamii, uhifadhi wa mazingira, usawa wa kijinsia, elimu, uchumi, ajira na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu," amesema Mlay.
Kwa upande wake, Mhandisi wa Miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Raya Majallah, amesema kuwa mikakati iliyopo inalenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania watakuwa wanatumia nishati safi ya kupikia.
Mhandisi Majallah amesema kuwa nishati safi ya kupikia ni ile yenye ufanisi, rahisi kutumia, inayopatikana kwa urahisi, salama na yenye gharama nafuu, huku isiyomuweka mtumiaji katika mazingira hatarishi yanayoweza kuathiri afya au kuchafua mazingira.
Aidha, amesema REA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa huduma za nishati safi ya kupikia ili kuwezesha Watanzania wengi zaidi kutumia nishati hiyo na kufikiwa kwa malengo yaliyowekwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Subira Mgalu, amesema kamati hiyo inaendelea kuisimamia Serikali katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya sekta hiyo, huku akieleza kuwa ametambua mchango wa Wizara ya Nishati na taasisi zake, ikiwemo REA, katika kufanikisha lengo la kuwafanya asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.
Naye Mkurugenzi wa WYFI na Mbunge Viti Maalum ( CCM), Mhe. Asha Baraka, ameishukuru REA kwa kutoa msaada wa mitungi 250 ya gesi ambayo itawanufaisha wananchi wa Mkoa wa Pwani.
Kwa upande wake, Meneja wa Elimu kwa Walipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), CPA Paul Walalaze, amesema Serikali imeendelea kutoa misamaha mbalimbali ya kodi, hususan Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), kwa waingizaji wa vifaa vinavyotumika katika matumizi ya nishati safi ya kupikia, ikiwemo mitungi ya gesi, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji na matumizi ya nishati hiyo nchini.
0 Comments