Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

ad728

TCB YAADHIMIA KUKUZA SEKTA YA VIWANDA NA MADINI

Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imesema imetenga takribani Shilingi trilioni 1.3 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa sekta za madini, viwanda na usafirishaji, hatua inayolenga kuunga mkono utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

Hayo yamesemwa leo, Septemba 9, 2026, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa TCB, Adam Mihayo, wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari pamoja na waandishi wa habari.

Mihayo amesema TCB imekuwa ikitekeleza maelekezo ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, ikiwemo kufanya maboresho katika sera za kifedha kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuchochea maendeleo ya sekta mbalimbali za kiuchumi.

“Tumetenga takribani Shilingi trilioni 1.3 ili kuwekeza katika sekta za madini, viwanda na usafirishaji, kwa lengo la kuchagiza ukuaji wa uchumi,” amesema Mihayo.

Ameongeza kuwa hatua hiyo inalenga pia kuongeza ufanisi wa mashirika na taasisi zinazohusika na uzalishaji na utoaji wa huduma, ili ziweze kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake, Kaimu Msajili wa Hazina, Lightnes Mauki, amesema kikao cha kutathmini utendaji wa mashirika ya umma kinatarajiwa kufanyika jijini Arusha, ambapo utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya mashirika hayo utapitiwa.





Post a Comment

0 Comments