Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

ad728

CHALAMILA AWATAKA WATENDAJI KUENDELEA KUTOA ELIMU YA MAJANGA KUKABILIANA NA EL NIÑO

Na Francisco Peter, Dar es Salaam

KUFUATIA utabiri wa kuwepo kwa mvua za El Niño, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka watendaji wa wilaya katika mkoa huo kuendelea kuboresha miundombinu pamoja na kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya uhifadhi wa taka, ili kupunguza athari za mafuriko.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Septemba 17, 2026, Chalamila amesema Serikali ya Mkoa huo pia imelenga kuboresha miundombinu ya shule na maeneo mengine muhimu kwa ajili ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua hizo.

“Natoa wito kwa Watanzania kuhifadhi chakula kipindi cha mvua za El Niño,” amesema Chalamila.

Ameongeza kuwa kumekuwa na changamoto ya baadhi ya wananchi kukaidi maagizo ya viongozi, hususan wakati wa mafuriko, ikiwemo kutotoka katika maeneo yaliyo hatarini.

Chalamila amesisitiza kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majanga na hatua za kuchukua ili kujikinga na athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo.

“Suala la mvua bado kuna ubishi kwa baadhi ya wananchi kuondoka kwenye maeneo hatarishi,” amebainisha Chalamila.


Post a Comment

0 Comments